Ma-DC walioapishwa watakiwa kugusa maisha ya wananchi


 Kaimu mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Yahaya Nawanda amewataka wakuu wa wilaya walioapishwa wakasimamie ipasavyo migogoro ya ardhi na kutekeleza ilani ya CCM kwa kusimamia miradi ya maendeleo iliyopo.

Pia amewataka wakurugenzi halmashauri, makamanda wa Polisi wa wilaya zote mkoani humo wasimamie watoto walioacha shule za msingi na sekondari warudi shuleni.

Hayo ameyasema leo Februari 1, 2023 baada ya kuapishwa kwa wakuu wa wilaya, akiwataka viongozi hao kuhakikisha watoto wote mkoani humo wanarudi shuleni na kutatua kero na migogoro ya ardhi.


"Muende kutenda haki kwa wananchi na kuhakikisha mnatatua kero zao, huku mkitekeleza ilani ya CCM na mkague miradi iliyopo katika wilaya zenu.

"Tatueni migogoro ya ardhi kwa kufuata haki, wananchi wana shida na wana kero nyingi, nendeni mkaguse maisha ya wananchi, vyombo vya dola vipo vizuri vitawasaidia, kasimamieni haki ya wananchi," amesema Nawanda.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita amesema atatekeleza majukumu yote kwa mujibu wa sheria bila kujali ukabila wala udini.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Profesa Siza Tumbo amesema maagizo yote yaliyotolewa na mkuu wa mkoa watayatekeleza ili kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi, wanarudisha watoto shule na kuhakikisha wanasimamia ipasavyo miradi ya maendeleo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments