Majaliwa atahadharisha video ukatili wa jinsia zinazorushwa mitandaoni


 Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ametoa wito kuacha kurekodi na kurusha mitandaoni matukio ya uvunjifu wa maadili, miiko ya taaluma kwani inaleta chuki kwa walimu na badala ya wahusika wachache.

Majaliwa ametoa wito huo leo Februari 2, 2023 bungeni wakati akitoa ufafanuzi na mwelekeo wa Serikali kuhusu taarifa na malalamiko kuhusu malezi na maadili.

Majaliwa ametoa wito kwa watu kutobeza jitihada zinazofanywa na walimu kote nchini na badala yake wawatie moyo hasa wale wanaozingatia miito yao.


“Licha ya mapungufu yao walimu kama nilivyoainisha awali walimu wamekuwa wakifanya mambo mengi na ya malezi kwa watoto wetu ambayo pengine hayazambazwi na kuyaona,”amesema.

Majaliwa ametoa wito kwa watu kutobeza juhudi zinazofanywa na walimu kote nchini na badala yake wawatie moyo hasa wale wanaozingatia miito, miiko na malezi.

“Nitoe wito kwa kwa jamii hasa wale wanaochukua na kupata matukio na kuyarusha katika mitandao kutofanya hivyo kwani kwa kufanya hivyo kunaleta chuki kwa walimu, taswira hasi kwa walimu wote badala ya wahusika wachache,”amesema.

Amesema pale yanapotokea yanapojitokeza utaratibu umewekwa kwa kutuma taarifa zake katika mamlaka husika ili hatua stahiki zichukuliwe huko huko badala ya kuleta taharuki kwa jamii nzima.

“Ninaomba nieleweke hapa lengo si kuficha taarifa bali na kuzuia chuki, taharuki na uhasama ndani ya jamii zetu si kwa walimu tu bali kwenye nyanja za mbalimbali, afya, vyombo vya ulinzi na usalama na maeneo mengine yanayofanana kama haya,”amesema.

Amesema anatambua siyo kusudio la walimu kuwadhuru wanafunzi lakini wakubaliane kuna udhaifu katika utoaji wa adhabu shuleni.

“Nitoe wito kwa maofisa elimu wa mikoa, maofisa elimu wa wilaya kuwakumbusha walimu wetu nchini juu ya mwongozo wa utoaji wa adhabu shuleni chini ya kifungu namba 61 cha Sheria ya Elimu pamoja na kanuni zake,”amesema.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments