Mbunge Ahoji Urasimu Maduka Ya Kubadilisha Fedha


 Mbunge wa Moshi Priscus Tarimo ameitaka Serikali kutoa wingu katika biashara ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni, akihoji sababu ya wafanyabiashara waliokidhi vigezo vipya kunyimwa leseni

Tarimo alikuwa akichangia leo Jumatatu Februari 6, 2023 wakati akichangia taarifa ya shughuli za Kamati ya Bunge ya Bajeti kwa Februari mwaka 2022 hadi Januari mwaka 2023.

Amesema Serikali ilifunga maduka ya kubadilisha fedha nchi na kuwanyang’anya pia fedha zao na nyaraka nyingine ambapo walisema kazi hiyo sasa itafanywa na benki.


Hata hivyo, Tarimo amesema kumekuwepo na watu wachache wamepewa leseni za kuendesha biashara hiyo na kwamba wako wafanyabiashara wengi ambao wamekidhi vigezo ambao hawapewi leseni.

“Wako ambao walikuwepo katika biashara hiyo na wapya ambao wamekidhi vigezo vyote vilivyowekwa katika maandishi lakini hawajapewa leseni. Nina ushahidi watu saba ambao wameomba, hawajakidhi vigezo sawa sawa,”amesema.

Amesema mtu huyo anakuwa analipa vizuri kodi au amewekeza kwenye maeneo mengine lakini hujibiwa hivyo na kwamba hajaelewa kwamba iko kwanuni ama utashi wa mtu.

Amesema hawasemei wafanyabiashara tu bali na waongoza watalii na wapagazi ambao wanakuwa wamelipwa kwa dola lakini wanapofika mjini hawawezi kubadilisha kwa sababu benki zinakuwa zimefungwa na hakuna maduka hayo.

Amehoji kwa nini leseni wamepewa watu wachache, hakuna majibu na watu wanateseka kwa sababu hakuna dola nchini.

Aidha, amesema katika maduka ya kubadilishia fedha za kigeni walikuwa wakibadilisha aina 20 za fedha za kigeni lakini kwenye benki wanabadilisha aina chache za fedha.

Aidha, amesema siku mbili zilizopita mchangiaji mmoja alisema kuna uhaba mkubwa wa dola katika benki nchini na kwamba wako wafanyabiashara pamoja na wabunge ambao wamekwenda benki wamechukua hadi wiki mbili kupata dola.


“Maeneo mengine unashauriwa kuwa mfanyabiashara unataka kufanya naye biashara umshawishi aweze kuchukua fedha nyingine kama Euro na nyingine, hatujapata majibu ya kutosha kuhusu upungufu wa dola unasababishwa na nini,” amesema.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments