Mbunge Ataka Kampuni za Simu Zifidie Wateja


 Mbunge wa Ulyankulu (CCM), Rehema Migilla ametaka kampuni za simu katika jimbo lake ambayo yamekuwa yakitoa huduma zenye kasi ndogo kuwafidia wananchi.

Akiuliza swali leo Jumatatu Februari 6, 2022 wakati akiuliza swali la nyongeza amesema huduma za simu na minara ya simu ni biashara na mwananchi anapotoa fedha zake kwa ajili ya kukunua vocha na mtandao anahitaji huduma nzuri.

Amesema, lakini cha ajabu kutokana na kasi ndogo ya minara katika eneo hilo huduma za simu mwananchi zinafikia muda wake kuisha ili hali ikiwa hajapata huduma aliyoikusudia.


“Je, hizi kampuni za simu ziko tayari kuwafidia hawa wananchi wetu ambao fedha zao zimetumika bila kupata huduma kwa sababu huu ni wizi kama wizi mwingine,”amehoji Rehema.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Methew Kundo amesema minara iliyopo katika maeneo hayo katika kata ya Nhwande inauwezo wa 2G pekee yake haijaanza kutoa huduma ya 3G.

Amesema mpango ni kuiboresha kufikia 3G hadi 4G na kwamba wakifikia katika kiwango hicho huduma itaweza kutolewa bila shida yoyote.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments