MBUNGE SILLO AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA DARAJA LA BILIONI 1.2 GICHAMEDA

Mbunge wa Babati Vijijini Daniel Sillo amesema Daraja la Gichameda kata ya Magugu lililogharimu Shilingi Bilioni 1.2 limekamilika na limeanza kutumika.

Kukamilika kwa daraja hilo linalounganisha Gichameda na vijiji vingine vya kata ya Magugu, kunatoa fursa kwa Wananchi kuweza kusafirisha mazao yao kwa urahisi.

Sillo amewataka Wananchi kuonesha uchungu kwenye kodi zao kwa kulitunza daraja hilo ili lidumu kwa muda mrefu.

Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo ambazo zimewezesha ujenzi wa daraja hilo.

Wananchi wa Kijiji cha Gichameda wamemshukuru Mbunge na serikali kwa kuharakisha ujenzi wa daraja hilo ambalo ni kiunganishi Muhimu na vijiji viingine.

Wanasema awali walikuwa wakiteseka kusafirisha mazao yao na kufuata huduma zingine za kijamii zikiwemo za Afya.

Katibu wa chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Babati Filbert Mdaki amempongeza Mbunge huyo kwa jitihada zake za kuwasemea wananchi bungeni na hatimaye daraja limepatikana.

Diwani wa kata ya Kisangaji Adamu Ipingika amesema daraja hilo lilikwamisha maendeleo kwa muda mrefu lakini kupitia Rais Samia na Mbunge wa Sillo fedha zimepatikana na daraja limejengwa.

TARURA Babati Vijiji wamesema awali walikuwa na shilingi milioni 200 tu lakini Mbunge huyo amefanikisha pesa zaidi kupatikana na kukamilisha daraja hilo

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments