MKUU WA WILAYA YA LUDEWA AONGOZA ZOEZI LA UGAWAJI WA PIKIPIKI KWA MAAFISA WATENDAJI WA KATA

                             

Februari 24, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanziva akiambatana na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ameshiriki zoezi la ugawaji wa pikipiki kwa Maafisa Watendaji wa Kata nane ambazo zimetolewa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Wakati wa zoezi hilo Mkuu wa Wilaya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa vyombo hivyo vya usafiri vitakavyo warahisishia watendaji kazi zao kutokana na jiografia ya maeneo mbali mbali ndani ya Wilaya ya Ludewa.

Amewaomba Watendaji wote walio kabidhiwa pikipiki siku ya leo kulinda Imani kubwa aliyo wapa Mheshimiwa Rais kwa kuwaletea pikipiki zitakazo wasaidia katika majukumu yao. 
Amesema Imani hiyo italindwa kwa matumizi mazuri ya hivyo vifaa kwani Mheshimiwa Rais aliahidi, na ametenda hivyo wanapaswa kuvitunza vifaa hivyo ili viwafae katika kazi zao kwa mda mrefu. 

DC Mwanziva amewaomba Watendaji kuzitumia pikipiki hizo katika kazi zilizo kusidiwa na kuboresha ufanisi wa utendaji wao. 

"Kupitia Pikipiki hizi zinakwenda kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wetu, jambo la kufanya siku nzima sasa tutatumia saa moja, tunamshukuru Mama Samia na tunaahidi kuwahudumia wananchi kwa kasi kubwa sasa" amewasilisha mmoja ya wapokeaji Maria Ngatunga Mtendaji wa Kata ya Madope.

Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ni miongoni mwa Halmashauri nchini iliyopata pikipiki 8 kati ya pikipiki 916 zilizotolewa na serikali na kuzigawa kwa Maafisa wa Kata.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments