MLIMA KIMELEMBE KUONDOLEWA, SERIKALI YATOA BL. 5.4

 Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe na Wilaya ya Ludewa zimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha sh. Bl. 5.4 kwaajili ya kupunguza mlima kimelembe ambao umekuwa ni kikwazo kwa shughuli za usafirishaji na hasa madini ya makaa ya mawe.


Akisoma taarifa ya mkakati wa ujenzi wa barabara ya Ludewa Manda Meneja wa TANROADS Mkoa wa Njombe Ruth Shaloah mbele ya kamati ya siasa Mkoa wa Njombe, kamati ya siasa wilaya ya Ludewa sambamba na viongozi wa serikali amesema kwa sasa tayari serikali imekwisha kutoa fedha kiasi cha sh.Bl. 5.4 zitakazo punguza mlima huo wenye umbali wa km. 4 kutoka asilimia 20 hadi asilimia 10.3.

Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa CCM Mkoani humo Deo Sanga amsema Rais Dkt. Samia Suluhu amekuwa akitoa mabilioni ya fesha ili kuiletea nchi maendeleo ambapo kwa wilaya ya Ludewa imekuja miradi mingi ya maendeleo.

"Rais wetu kila kukicha anatuletea fedha Mabi na Mabii hihvyo tunakila sababu ya kumpongeza kwani juhudi zake za maendeleo zinaonekana kwa vitendo". Amesema Sanga.

Hata hivyo kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amesema kuondolewa kwa kikwazo hicho cha mlima.

 kutakwenda kuokoa maisha ya watu kwani kuna watu wamepoteza maisha yao huku wengine wakipata ulemavu kutokana na ajali zilizokuwa zikijitokeza mahala hapo.

Naye mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amesema barabara hiyo ya Manda Ludewa ina umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya Ludewa hivyo ameishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu kwa kutoa fedha za kurahisisha mawasiliano hayo ya barabara.

" Barabara ni moja ya chanzo cha maendeleo na kukua kwa uchumi, hivyo endapo barabara hiyo itakamilika itarahisisha usafirishaji makaa ya mawe, biashara mbalimbali za mazao ya chakula kwakuwa kikwazo kinachozuia kupita magari makubwa kwa urahisi kitakuwa kimekwisha ondolewa". Amesema Mwanziva.








TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments