Naibu Waziri wa Utamaduni azipa maagizo halmashauri

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul ametoa rai kwa Halmashauri zote nchini kuzingatia matakwa ya Sera ya Michezo ya kujenga na kukarabati miundombinu ya michezo.

Waziri Gekul ametoa rai hiyo Februari 09, 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Masasi, Geofrey Mwambe aliyetaka kujua ni lini Serikali itaboresha Uwanja wa Mpira wa Boma uliopo Masasi kwa kiwango kinachofaa ili kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wa Masasi

."Kwa mujibu wa Sera ya Michezo ya mwaka 1995 ibara ya 1-4, Jukumu la ujenzi wa miundombinu ya michezo ni jukumu la Serikali Kuu, Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Taasisi, Mashirika na watu binafsi.


Hivyo nitoe rai kwa Halmashauri nchini kuzingatia matakwa ya sera hii," ameeleza  Gekul.Gekul amesisitiza kuwa halmashauri nchini zinatakiwa kutenga fedha kwa ajili ya shughuli za michezo pamoja na kukarabati miundombinu na kujenga viwanja kama zilivyofanya Halmashauri za Ruangwa, Geita, Nyamagana na Bukoba.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments