NIMEFURAHISHWA NA MIRADI YA KIMAENDELEO-MAJALIWA


waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama michoro ya Mradi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasicha Ruangwa wakati alipokagua mradi huo, Februari 22, 2023. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Frank Chonya. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) 

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruangwa ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake, February 22, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wakati alipowasili kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruangwa mkoani Lindi kukagua ujenzi wa Jengo la Utawala la Sekondari hiyo, Februari 22, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama madawati wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa Jengo la Utawala la Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruangwa, Mkoani Lindi, Februari 22, 2023. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Frank Chonya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana, Ruangwa baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Utawala la shule hiyo Mkoani Lindi, Februari 22, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

*****************************

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema anafurahishwa na mafanikio makubwa ya utekelezwaji wa ujenzi miradi mbalimbali ya maendeleo yanayoonekana katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

“Wana-Ruangwa lazima tuendelee kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Haya ni mafanikio makubwa, Ruangwa kwa maendeleo inawezekana.”

Amesema hayo leo (Jumatano, Februari 22, 2022) baada ya kukagua ujenzi wa jengo la utawala shule ya Sekondari ya Wasichana Ruangwa (Ruangwa Girls) pamoja na madarasa katika Shule ya Sekondari ya Kitandi wilayani Ruangwa.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia anaridhia kutoa fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu mbalimbali ya utoaji huduma za jamii hapa nchini hivyo ni jukumu la kila wananchi ni kuitunza ili ilete faida anayoikusudia

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wanafunzi kwamba wajitahidi kufanya vizuri kwenye masomo yao “Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameweka mkazo katika elimu, ambayo inatolewa bure kuanzia awali hadi kidato cha sita”

“Jitahidini kufanya vizuri kitaaluma, mjitambue nyie ni wanafunzi na hivyo mjiepushe na vishawishi vyovyote vitakavyokwamisha maendeleo yenu kitaaluma. Wananchi tuwalinde watoto wetu ili watimize ndoto zao. Mtoto wa mwenzio ni wako.”

Pia, Waziri Mkuu amewataka wananchi kuacha kuvamia maeneo ya karibu kwa kuwa Serikali imeyahifadhi kwa ajili matumizi ya baadae ya taasisi husika. “Hapa palikuwa pori hapakuwa na shamba pasiguswe.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekagua ujenzi wa madarasa ya ghorofa yanayojengwa katika shule ya msingi Likangara, ambapo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kwa ubunifu wa mradi huo. Mradi huo unahusisha vyumba vinane vya madarasa, matundu 24 ya vyoo na ofisini nne.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments