NTIBAZONKIZA ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MASHABIKI

MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Saido Ntibazonkiza ameibuka kuwa mshindi wa tuzo ya Mchezaji bora wa mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month) mwezi Januari, 2023.

Ntibazonkiza ambaye ni raia wa Burundi amewashinda Wachezaji wa timu hiyo, Shomari Kapombe na Mohammed Hussein (Zimbwe Jr) na kuondoka na kitita cha zawadi nono ya Tsh. Milioni 2/- na zawadi ya ‘Trophy’.

Akizungumza, Februari 6, 2023 jijini Dar es Salaam baada ya kupokea tuzo hiyo, Ntibazonkiza ameshukuru M/Mungu kushinda zawadi hiyo ambayo mara zote mashabiki wa timu hiyo wanampiga kura kuchagua Mchezaji husika kila mwezi.

Ntibazonkiza ameshukuru Wachezaji wenzake wa Simba SC, Benchi la Ufundi sanjari na Klabu yote kuwezesha kuibuka mshindi na kunyakua tuzo hiyo ya mwezi ambayo mara zote inakuwa na ushindani wa wachezaji watatu huku Mashabiki wakipiga kura kuchagua mshindi.

“Nashukuru kupata tuzo hii, nawashukuru Emirate Aluminium kwa kutusapoti sisi Wachezaji kwa kutambua mchango wetu tukiwa uwanjani, tunaomba waendelee na moyo huu ili kutupa hamasa sisi Wachezaji kufanya vizuri zaidi hata Mashabiki tunawashukuru kutupigia kura na kutupa hamasa sisi Wachezaji kufanya vizuri zaidi”, amesema Ntibazonkiza.

Kampuni ya Emirate Aluminium Profile kila mwezi inaendelea kutoa tuzo kwa Wachezaji wa Simba SC ambayo wanashindanishwa kwa mwezi husika, huku wakibainisha kuja na bidhaa bora ambayo ni nzuri na bora kwa watumiaji wa bidhaa hizo za Kampuni hiyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments