RAIS SAMIA AWATAKA VIJANA KUWA NA ARI YA KULITUMIKIA TAIFA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) na ZAHLIFE kutoka Zanzibar pamoja na Wale wanaowakilisha Serikali za Wanafunzi kutoka Taasisi za Elimu ya Juu, Tanzania Bara na Zanzibar kwenye Mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

………………………………

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa vijana kuwa tayari kulitumikia taifa ili kudumisha amani, mshikamano na kuleta maendeleo.

Rais Samia ametoa wito huo leo wakati akizungumza na wawakilishi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) na Zanzibar (ZAHLIFE) katika viwanja vya Ikulu, Chamwino.

Aidha, Rais Samia amewataka wanafunzi kuwa na ufahamu kuhusu mwelekeo wa nchi na aina ya Taifa tunalotaka kulijenga ambalo linajitegemea kiuchumi.

Vile vile, Rais Samia amesema Wizara ya Elimu inapitia mitaala ambayo itaongeza ubora na kuzingatia ujuzi ili wahitimu waweze kujitegemea baada ya kuhitimu masomo yao.

Hali kadhalika, Rais Samia amewataka vijana wa vyuo vikuu kuelewa changamoto kubwa za kidunia zikiwemo mabadiliko ya tabianchi na usalama wa chakula na kutoa elimu kwa jamii kuhusu mikakati ya kukabiliana nazo.

Rais Samia pia amewataka vijana kuwa mstari wa mbele kuielimisha jamii umuhimu wa kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji na kuwahimiza wananchi kuongeza uzalishaji ili pia kunufaika na soko kubwa la bidhaa za chakula duniani.

Serikali inafanya jitihada mbalimbali ili kuinua elimu ya juu ambapo imekamilisha mkataba na Benki ya NMB wa thamani ya shilingi bilioni 200 ili wazazi ambao mishahara yao inapitia benki hiyo waweze kukopa kwa ajili ya vijana wao.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments