Wananchi mkoani Ruvuma wamemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu kwa
kutoa fedha ambazo zimewezesha kujengwa kwa sekondari mpya zenye
mazingira ya kuvutia katika Halmashauri zote nane.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Grace Quietine amesema
Rais ametoa shilingi milioni 470 kujenga sekondari mpya katika Kata ya
Lusonga ambayo imekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.
Amesema kiasi hicho cha fedha kimewezesha kujenga jengo la
utawala,vyumba nane vya madarasa,maabara tatu,jengo la TEHAMA,jengo
la maktaba,vyoo matundu 20 na sehemu ya kunawia maji mikono
wanafunzi.
Amesema tayari wanafunzi wa kidato cha kwanza wamesajiriwa na kuanza
masomo ambapo hivi sasa shughuli za umaliziaji zinaendelea zikiwemo za
kuweka mfumo wa gesi na maji katika majengo ya maktaba na kwamba
Halmashauri pia imeongeza fedha za kukamilisha mradi huo ambapo hadi
sasa zaidi ya shilingi milioni 492 zimetumika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru
Chiza Marando amesema anamshukuru Rais kwa upendeleo wa pekee
wa kuwapatia kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kujenga sekondari mpya tatu za
mfano katika wilaya hiyo ambazo zimekamilika na kuanza kuchukua
wanafunzi wa kidato cha kwanza.
Amesema kila sekondari imepewa shilingi milioni 470 na kuzitaja sekondari
hizo kuwa zimejengwa katika kata za Nakayaya,Majimaji na Lukumbule na
kwamba kila shule imejenga jengo la utawala,madarasa
nane,vyoo,samani,maabara tatu,jengo la TEHAMA na maktaba.
“Shule zote tatu zinaendelea na hatua za ukamilishaji,lakini tumeshazisajiri
na tumeshazifungua,wanafunzi wanaendelea kusoma, tunamshukuru sana
Rais kwa kutumbuka Tunduru’’;alisema Marando.
Hata hivyo amesema kufunguliwa kwa shule hizo kumepunguza kero ya
wanafunzi kwenye kata hizo kusafiri umbali mrefu kufuata sekondari.
Rais Samia pia ametoa shilingi milioni 470 kujenga sekondari mpya katika
Kata ya Msisima Halmashauri ya Namtumbo na kwamba sekondari hiyo
imefunguliwa na wanafunzi wameanza masomo.
Halmashauri nyingine ambazo zimepata fedha za ujenzi wa sekondari
mpya ni Manispaa ya Songea katika Kata ya Mshangano zimetolewa
shilingi milioni 470 kujenga sekondari ya Luhira.
Kata nyingine ni ya Amanimakoro Halmashauri ya Mbinga,Kata ya Riwundi
wilaya ya Nyasa,Kata ya Lituta Halmashauri ya Madaba na Kata ya Kizuka
Halmashauri ya wilaya ya Songea.
Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 7.7 kujenga sekondari mpya 11
katika Mkoa wa Ruvuma kupitia program ya kuboresha Elimu ya sekondari
nchini (SEQIUP).Jengo la Utawala na vyumba vya madarasa katika sekondari mpya Kata ya Nakayaya wilayani Tunduru mkoani Ruvuma ambayo serikali imetoa shilingi milioni 470 kutekeleza mradi huo
Jengo la Utawala na vyumba vya madarasa katika sekondari mpya Kata ya Nakayaya wilayani Tunduru mkoani Ruvuma ambayo serikali imetoa shilingi milioni 470 kutekeleza mradi huo
Jengo la utawala na vyumba vya madarasa katika sekondari mpya kata ya Lusonga Halmashauri ya Mji wa Mbinga ambapo serikali imetoa shilingi milioni 470 kutekeleza mradi huo
Baadhi ya wanafunzi katika sekondari ya Msisisma wilayani Namtumbo wakiwa wameanza
Bbaadhi ya vyumba vya madarasa katika sekondari mpya Kata ya Msisima Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ambapo serikali imetoa shilingi milioni 470 kujenga sekondari hiyo
Jengo la Utawala katika sekondari mpya ya Luhira kata ya Mshangano Manispaa ya Songea.
0 Comments