SERIKALI YADHAMIRIA KUTEKELEZA MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA KWA MANUFAA YA TAIFA

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.)ameihakikishia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara  na Mazingira kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza Mradi wa Kimkakati wa Liganga na Mchuchuma kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.


Aidha, Dkt. Kijaji amewahakikishia wajumbe hao kuwa Serikali imekamilisha kuhakiki ardhi na mali za wananchi watakaopisha Mradi  na imejipanga kulipa fidia kwa wakazi wa maeneo ya mradi huo ili kurahisisha utekelezaji wa mradi huo kuanza. 

Dkt. Kijaji ameyasema hayo wakati wa Semina ya kuwaelimisha Wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu  utekelezaji wa Mradi wa Kimkakati wa Liganga na Mchuchuma, Februari 09, 2023, Bungeni, Jijini Dodoma. 

Wakichangia kwa nyakati tofauti Wajumbe wa Kamati hiyo  wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. David Mwakiposya Kihenzile wamesema Mradi huo wa Kimkakati unapaswa kuanza kutekelezwa mapema iwezekanavyo ili kuleta manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Vilevile, Wajumbe wa Kamati hiyo walitoa maoni na mapendekezo mbalimbali yaliyolenga kusaidia jitihada za kukamilisha taratibu za kuanza kutekeleza Mradi huo kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah aliieleza Kamati hiyo kuwa utekelezaji wa Mradi huo wa Kimkakati utafuata  taratibu na Sheria  zinazosimamia Uwekezaji, Madini, Kodi na Raslimali za nchi zilizopo ili kuhakikisha Mradi huo unaleta manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Naye, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Dkt. Nicolaus Shombe akitoa elimu kwa wajumbe hao amesema NDC inatekeleza miradi  ya  kielelezo  (Flagship  projects)  na  miradi  ya 
 kimkakati  ikiwemo Mradi unganishi wa Mchuchuma na Liganga, Mradi  wa  chuma  ghafi wa  Maganga  Matitu  na  Makaa  ya  Mawe  Katewaka na  Ngaka iliyopo pamoja na miradi mingine iliyopo nchini.
WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ,akizungumza wakati wa Semina ya kuwaelimisha Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira  kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Kimkakati wa Liganga na Mchuchuma, iliyofanyika leo Februari 09, 2023, Bungeni, Jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Mwakiposya Kihenzile,akizungumza wakati wa Semina ya kuwaelimisha Wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Kimkakati wa Liganga na Mchuchuma, iliyofanyika leo Februari 09, 2023, Bungeni, Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah,akieleza Kamati kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Kimkakati wa Liganga na Mchuchuma, iliyofanyika leo Februari 09, 2023, Bungeni, Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Dkt. Nicolaus Shombe akitoa elimu kwa wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu miradi ya kielelezo (Flagship projects) na miradi ya 
kimkakati ikiwemo Mradi unganishi wa Mchuchuma na Liganga, Mradi wa chuma ghafi wa Maganga Matitu na Makaa ya Mawe Katewaka na Ngaka inayotekelezwa na NDC




Wajumbe  wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakiendelea kufuatilia  mada ,mbalimbali wakati wa Semina ya kuwaelimisha Wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Kimkakati wa Liganga na Mchuchuma, iliyofanyika leo Februari 09, 2023, Bungeni, Jijini Dodoma.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments