Serikali Yataka Ushirikiano Wadau Wa Habari

Serikali imewataka wadau wa habari nchini kuongeza ushirikiano katika kukuza sekta hiyo kwa maendeleo ya Taifa.

Hayo yameelezwa jana Februari 18, 2023 na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kundo Mathew aliyezungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari Nape Mosses Nnauye katika hafla ya utoaji tuzo za umahiri katika tasnia ya Uhusiano na Umma na Mawasiliano  iliyofanyika jijini hapa.

Hafla hiyo iliyoandaliwa na Chama cha Maofisa Uhusiano na Umma na Mawasiliano nchini (PRST) ikilenga kutambua kazi kubwa zinazofanywa na Maafisa hao kwa mashirika, jamii na Taifa. kupongeza na kuchochea uwajibikaji kwa Maafisa Mawasiliano nchini. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwamo viongozi wa Chama cha Maofisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO), viongozi wa Jukwaa la Wahariri, Baraza la Habari Tanzania (MCT), Chama cha Waandishi wa Habari za Wanawake (TAMWA), MISA TAN, Viongozi kutoka serikani na vyuo vikuu nchini.


“Ni vema mkatambua kwamba sisi sote tunajenga nyumba moja hakuna haja ya kugombania fito. Tukiendeleza ushirikiano huu tutapiga hatua kubwa kimaendeleo na kutimiza malengo yetu kwa haraka zaidi.

“Mimi na watendaji wote wa Wizara tukiongozwa na Mheshimiwa Waziri Nape Nnauye muda wote tunaongozwa na falsafa ya kufanya kazi kwa ushirikiano,” amesema.

Kuhusu kuhakikisha kwamba tasnia ya Uhusiano na Mawasiliano ya Umma inatambuliwa na kupewa heshima inayostahili, alisema Wizara hiyo iko tayari kupokea na kufanyia kazi mchakato wa rasimu ya Sheria ya kutambua taaluma hiyo.

Akizungumza wakati wa kuwataja washindi katika tuzo hizo, Jaji Mkuu wa jopo la Majaji Jossey Mwakasyuka, amesema kwa tuzo zimegawanyika katika makundi mawili (Taasisi na wanataaluma mmoja mmoja) katika vipengele mbalimbali.


Elimu kwa Umma, mshindi wa kwanza ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mshindi wa pili  Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wa tatu ni mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA).

Katika kundi la Uhusiano na vyombo vya Habari, mshindi wa kwanza ni  Mamlaka ya Usimamizi wa Maji na Nishati (Ewura), wa pili ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mshindi wa tatu ni Benki ya CRDB.

Kwa upande wa mashirika na kampuni zinazosaidia jamii kwa kutumia mfumo wa jamii (CSR), mshindi kwanza ni Benki ya NMB, wa pili ni kampuni ya Geita Gold Mine na tatu ni Shrika la Maendeleo ya Petrol (TPDC).

Kwa upande wa tuzo kwa taasisi, mashirika na kampuni zenye muundo mzuri wa Idara za Mawasiliano mshindi pekee ni NMB, huku tuzo za mashirika, taasisi na kampuni zenye mfumo mzuri wa kutabiri na kudhibiti majanga hakuna aliyekidhi vigezo.

Kwa tuzo maaluma zilizotolewa kwa maofisa Uhusiano na Mawasiliano katika sekta mbalimbali, Nelly Msuya Kutoka Dawasa alishinda katika sekta ya Maji na Usafi wa mazingira, huku sekta ya Elimu akiongozwa  ni Bw.Living Komu kutoka kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania  (SAUT), Mwanza.

Kwa upande wake Sekta na Nishati na Gesi, aliyeshinda ni Titus Kaguo kutoka EWURA, Sekta ya Michezo aliyeshinda ni Sabrina Msuya kutoka Sports Pesa na kwa upande wa Afya aliyeshinda ni Patrick Mvungi kutoka taasisi ya Mifupa (MOI).

Nyingine ni Sekta ya Madini iliyokwenda kwa Stephen Mhando kutoka GGM, Sekta ya bima aliyeshinda ni Oyuke Phostine kutoka Mamalaka ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA).


Katika Sekta ya Fedha mshindi ni Vincent Mnyanyika kutoka benki ya NMB, kwa masirika ya kimataifa aliyeshida ni Magreth Edwin kutoka UNCDF na Mashirika yasio ya kiserikali (NGO) aliyeshinda ni Oscar Kimaro kutoka Marie Stop.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments