SIMBA SC YASHINDWA KUFURUKUTA MBELE YA HOROYA AC, YACHAPWA 1-0 UGENINI

 

KLABU ya Simba imeshindwa kutamba katika mchezo wake wa kwanza hatua ya makundi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuambulia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Horoya AC ya nchini Guinea.

Horoya AC ilianza kupata bao kupitia kwa nyota wao kutoka nchini Senegal, Pape Ndiaye aliefunga kwa kichwa dakika ya 18 kipindi cha kwanza.

Katika mchezo huo licha ya kipindi cha kwanza Horoya AC kutawala mchezo, kipindi cha pili Simba walirudia na hali ya kutaka kurudisha bao na kuweza kupata ushindi kwenye mchezo huo lakini matumaini yakayeyuka baada ya Nahodha wao John Bocco kukosa nafasi nyingi za wazi.

Kwenye mchezo huo ambao ulipigwa katika dimba la Lansana Conte General nchini Guinea, Aishi Manula alionesha umwamba wake kwa kuchomoa penati ambayo ilisababishwa na Josh Onyanga kuushika mpira ndani ya boksi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments