Tembo wanaosumbua Lindi wafungwa GPS

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mohamed Moyo ameongoza zoezi la ufungaji visukuma mawimbi ‘GPS Satellite’. Collars" kwa makundi ya Tembo wanaosumbua wananchi katika Vijiji vya Wilaya za Nachingwea, Liwale na Tunduru.

Zoezi hilo linaloendeshwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), kwa kushirikiana na viongozi wa Wilaya na vijiji lilianza kutekelezwa Februari 10, 2023.

Lengo ni kusaidia kupata taarifa za wakati kuhusu mienendo na mahali yalipo makundi ya tembo na hivyo kurahisisha ufuatiliaji na kuzuia wanyamapori hao wasilete madhara kwa watu, makazi na mashamba yao.


Katika zoezi hilo jumla ya visukuma mawimbi vitano vilitarajiwa kufungwa kwenye makundi ya tembo, ambapo hadi kufikia Februari 12, 2023 jumla ya visukuma mawimbi vitatu vilifungwa kwenye makundi matatu ya tembo katika maeneo ya Milola/Mitamba (Wilaya ya Lindi vijijini), Mkutano (Liwale) na Ngolanga ambayo ni shoroba ya Selous - Niassa (Tunduru).

Visukuma mawimbi viwili vilivyobaki vinatarajiwa kufungwa katika maeneo ya Wilaya hiyo yenye changamoto kubwa zaidi.

Vilevile, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (Tawiri) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyapori Tanzania (Tawa) zitaendelea kufunga visukuma mawimbi kwenye makundi mengine ya tembo ili kuwezesha vikosi vya askari wanaofanya doria za kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu kufika kwa haraka katika maeneo ya karibu na vijiji tembo hao watakapoonekana.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea ameipongeza Serikali kupitia taasisi zake za Tawiri na Tawa kwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa ikiwa ni pamoja na kuongeza matumizi ya teknolojia katika kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu.

Pia, amebainisha kuwa uongozi wa wilaya uko tayari kuendelea kushirikiana na wataalamu wa uhifadhi katika kutatua changamoto hii.

Chanzo Na Mwananch

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments