Mkurugenzi Wa Kijiji cha Nyuki Bw. Philemon Kiemi pamoja na Mjumbe Wa Mkutano Mkuu CCM Bw. Ahmed Misanga Leo Wamezindua Upandaji miti elf 5000 Pembezoni Mwa Barabara ya Kisaki - Wilayani Ikungi Mkoani Singida na ndani ya shamba la ufugaji nyuki Linalo Milikiwa na Kampuni ya Kijiji cha nyuki.
Mkurugenzi wa Kijiji Cha Nyuki Bw Kiemi Amesema Kijiji cha nyuki tumeamua kuwekeza katika upandaji miti kwa kuzingatia kwamba Nyuki wana mchango Mkubwa katika maisha ya binadamu na mazingira kwa ujumla na hasa umaarufu wake wa kuzalisha chakula Kisichooza ambacho ni Asali na mazao yake mengine...
Bw Kiemi Ameendelea kusema kuwa Manufaa ya nyuki yanaenda mbali zaidi ya Asali hadi kwenye uzalishaji wa vyakula mbalimbali vya kawadia , Dawa na pia utunzaji wa mazingira kwani nyuki ni sehemu muhimu ya ukuaji uendelevu wa mimea kutokana na Uchavushaji (Pollination).
Aidha Bw. Kiemi Amesema Kuwa Kwa sasa wadudu hao wako hatarini kutokana na uchafuzi na uharibifu wa misitu na mazingira kwa kuzingatia Hilo kampuni ya Kijiji cha Nyuki Tumeamua kuwekeza katika upandaji miti elf 10 kila mwaka na kuhaikisha miti Hiyo Inakuwa.
0 Comments