Waliopata Division I St Anne Marie Academy Waula

 WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne wanaandaliwa ziara ya kutembelea mbuga za wanyama za Mikumi na Ngorongoro kama motisha ya kuwafanya wengine nao wafanye vizuri.

 Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa shule hiyo, Gladius Ndyetabura wakati akizungumza na gazeti hili kuhusu matokeo ya kidato cha nne ambapo wanafunzi 103 wa shule hiyo walifanikiwa kupata daraja la kwanza.

 Alisema kwenye mtihani huo wanafunzi 40 walipata daraja la pili na wanafunzi saba pekee ndio wamepata daraja la tatu.

 “Haya ni matokeo mazuri sana kwetu ukizingatia tulikuwa na wanafunzi wengi lakini wote wamefanikiwa kupata nafasi ya kuendelea na kidato cha tano ndiyomaana tunawaandalia safari hii ya kwenda Mikumi na Ngorongoro kama motisha kwao na kwa wenzao ili wapate ari ya kufanya vizuri,” alisema

 Aliwapongeza na kuwashukuru walimu wa shule hiyo ambao wamefanyakazi kubwa usiku na mchana kuhakikisha wanafunzi wote wanafaulu kwa ufaulu wa  juu na alimshukuru pia Mkurugenzi wa shule hiyo, Dk. Jasson Rweikiza kwa ushirikiano ambao amekuwa akiutoa kwa walimu.

 Alitaja siri ya mafanikio hayo kuwa ni shule kuwa na mazingira mazuri ya wanafunzi kusomea ikiwemo maktaba ya kisasa  na maabara iliyosheheni vifaa vya kutosha pamoja na walimu mahiri wanaojua kazi yao

“Wanafunzi wetu wanakula milo minne kwa siku na tuna mashamba ya mboga mboga na matunda kwa hiyo wanakula mlo kamili na mazingira kwa ujumla ni mazuri sana kuwawezesha kujisomea muda wowote,” alisema

 Alisema shule hiyo imedhibiti ulinzi kwa kuweka walinzi 46  wenye mafunzo wakisaidiwa na mbwa wao ambao wamekuwa wakizunguka usiku na mchana kuhakikisha kunakuwa na usalama.

 “Hawa walinzi wetu wamepata mafunzo ya kisasa kiasi kwamba hata ukitokea moto wakotayari kuuzima ndani ya dakika chache kwa hiyo wazazi msiwe na wasiwasi kuhusu taaluma na suala la usalama,” alisema

 Mwaka 2021 St Anne Marie Academy ilitoa mwanafunzi bora kitaifa, Elulei Haule anayesoma kidato cha kwanza shule ya Marian Boys ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

 Akizungumza kwenye mahafali ya kidato cha nne mwaka huu, Mkurugenzi wa shule hiyo, Dk. Rweikiza, alitangaza kwamba hakuna mwanafunzi yoyote wa shule hiyo atakayefukuzwa kwasababu ya kufiwa na wazazi wake na kukosa ada.

 Alisema wakati wa mlipuko wa korona mtandao wa shule zake ulipoteza wazazi 46 lakini hakuna aliyewahi kufukuzwa kwa kushindwa kulipa ada na wanaendelea.

 

“Nilisema wakati ule tulipopoteza wazazi 46 na narudia leo kusisitiza kwamba msimamo bado ni ule ule. Hata baada ya korona watu bado wanakufa kwasababu hakuna anayejua kesho yake,” alisema na kuongeza.

 “ Kama mwanafunzi yuko shule ya msingi atamaliza darasa la saba bila kulipa ada na kama yuko sekondari atamaliza kidato cha nne bila kulipa ada

Mkuu wa shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri, Gladius Ndyetabula, akimpa zawadi ya ngao mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne wa shule hiyo ambayo kwenye matokeo hayo wanafunzi 103 wa shule hiyo wamepata daraja la kwanza na 40 daraja la pili na saba kupata daraja la tatu. 

Mkuu wa shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri, Gladius Ndyetabula, akimpa zawadi ya vitabu mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne wa shule hiyo ambayo kwenye matokeo hayo wanafunzi 103 wa shule hiyo wamepata daraja la kwanza na 40 kupata daraja la pili na saba daraja la tatu
 Wahitimu wa shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha na Mkuu wa shule hiyo, Gladius Ndyetabula, wakati walipokwenda shuleni hap leo kwaajili ya michezo mbalimbali. Kwenye matokeo ya kidato cha nne wanafunzi 103 wa shule hiyo walipata daraja la kwanza na wengine 40 daraja la pili
Wahitimu wa shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam wakiwa na furaha baada ya kuahidiwa kupelekwa mbuga za mikumi na Serengeti kufuatia wanafunzio 103 wa shule hiyo kupata daraja la kwanza na wengine 40 kupata daraja la pili

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments