Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Martha Mlata amewataka wazazi na walezi kuwa Karibu na watoto ili Kuwanusuru dhidi ya ukatili ambao wamekuwa wakifanyiwa na kuleta madhara makubwa kwa kundi hilo na Jamii kwa ujumla.
Mlata amesema Hayo katika kijiji cha Minyughe Wilayami Ikungi Mkoani Singida kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi kwa Mkoa wa Singida ambapo amewataka wazazi kuwafuatilia mienendo ya watoto ili kuwanusuru dhidi ya ukatili huo.
Kuhusu utekelezaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi, Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba amesema serikali bado inaendelea kutekeleza ilani ya chama hicho ikiwemo sekta ya nishati ambapo kabla ya mwaka 2025 vijiji 441 vya mkoa wa Singida vitakuwa vimepata umeme.
Piter Serukamaba ameendelea kusema kuwa Viongozi na Watendaji Wa mkoa Wa Singida wamejiwekea utaratibu wa ktoka maofisini na kwenda Kusikiliza kiro Na malalamiko mbali mbali Kwajili Ya Kizitatua ,Kuziwekea ratiba za utatuzi Kwa Viongozi na watendaji wa ngazi ya mkoa,Wilaya,Taarafa, Kataa na Vijiji/ Mitaa
Aidha Serukamba Amewaomba Vingozi Wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Kuungana Katika jambo Hilo Ili Kupunguza maswali ya wananchi hasa kwa viongozi wa kitaifa Wanapotembelea mkoa na wilaya Kwa Ujmla.
Suala La Mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali hapa nchini likamuibua Mbunge wa Singida Magharibi Elibarick Kingu (Kepteni) na kuitaka serikali kutoa msimamo wake ili kuwapunguzia ugumu wa maisha.
Kwa Upande Wa Katibu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Wa Singida Bi Lucy Boniphace Shee Aliwakaribisha Viongozi Mbali Mbali Katika Maadhimisho hayo, kwa Mkoa wa Singida yamefanyika Katika kijiji cha Minyughe Wilayani Ikungi pia na viongozi wa Serikali wakiemo wakuu wapya wa Wilaya ya Manyoni na Ikungi.
Na Abdul Bandola Singida.
0 Comments