Waziri Chana Aagiza BASATA Kuandaa Mwongozo Wa Programu Ya Sanaa Mtaa Kwa Mtaa

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuandaa mwongozo wa kutekeleza Programu ya Sanaa mtaa kwa mtaa ili kuibua vipaji vingi kuanzia ngazi ya chini.


Mhe. Chana ametoa maagizo hayo Februari 21, 2023 alipofanya ziara katika Baraza hilo ambapo amesisitiza Sekta ya Sanaa kuendelea kuongeza ukuaji katika Pato la Taifa

"Natoa rai kwenu BASATA kuwa na takwimu sahihi kuhusu idadi ya Wasanii katika aina zote za Sanaa ambazo zitakuwa zinahuishwa kila baada ya muda mfupi na zitasaidia katika upatikanaji wa mikopo pamoja na udhamini kutoka taasisi mbalimbali," amesisitiza Mhe. Chana.

Amesisitiza Baraza hilo kuendelea kutoa elimu kwa wadau wa Sanaa katika kufanya Sanaa zinazoelimisha, kuburidisha bila kuvunja maadili ya kitanzania.

Awali, akimkaribisha Waziri, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Pauline Gekul amesisitiza Baraza hilo kutoa kipaumbele katika sanaa nyingine kama linavyofanya katika muziki pamoja na kutoa fursa kwa vikundi mbalimbali vya maeneo tofauti kushiriki matamasha ya kimataifa.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Kedmon Mapana amesema Baraza hilo limefanikiwa kuanzisha mfumo wa usajili wa Wasanii Kidijitali, pamoja na kurejesha Tuzo za Muziki.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments