YANGA SC YAJICHIMBIA KILELENI NBCPL, YAINYUKA NAMUNGO FC 2-0

 

KLABU ya Yanga imefanikiwa kuichapa Namungo Fc kwa mabao 2-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Yanga Sc imefanikiwa kuchukua pointi tatu muhimu na kufanikiwa kujikusanyia jumla ya Pointi 59 na kuwa kileleni kwa tofauti ya pointi sita na ambaye anamfuate nyuma akiwa na pointi 53.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Dikson Job kipindi cha kwanza na kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele kwa 1-0 na bao la pili limefungwa na nyota kutoka Burkanafaso Aziz Ki mnamo dakika ya 50

Post a Comment

0 Comments