Afikishwa mahakamani kwa kuwaingilia mbuzi wa jirani kimwili


 Mkulima na mkazi wa Kijiji cha Naibili wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro, Emmanuel Kilenga ( 22) amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Siha Machi 17, 2023 akikabiliwa na shtaka la kuandama wanyama kesi iliyosajiriwa kwa namba CC 35/2023.

Akisoma mashtaka mahakamani hapo Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Kulwa Mungo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Elibahati Ndewario Petro, inadaiwa kuwa mtuhumiwa aliingia katika zizi la mifugo na kumuingilia kimwili mbuzi, tukio lilitokea Machi 14 mwaka huu majira ya usiku.

Kwa upande wake mshtakiwa hakuwa na cha kusema mahakamani hapo ambapo shauri liliahirishwa hadi Mach 30 mwaka huu ambapo shauri litakuja kwa hatua ya usikilizwaji wa awali. Hata hivyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa mahabusu.


Taarifa zaidi kutoka kwa majirani zinadai kuwa mtuhumiwa amekuwa na tabia ya kuingilia wanyama wa majirani hali iliyopelekea baba yake mzazi kufidia wanyama mara kwa mara.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments