CCM Yaiagiza Wizara Ya Kilimo Kuongeza Vituo Vya Mawakala Wa Mbolea Ili Kuondoa Changamoto Ya Upatikanaji Wake

Wizara ya Kilimo imeagizwa kuongeza vituo vya mawakala wa mbolea kwa ajili ya kuuza mbolea kwani hivi sasa wakulima wamekuwa wakitoa fedha nyingi kugharamia mbolea ili iwafikie, hivyo njia pekee ni kuongeza vituo vya mawakala.

Maagizo hayo yametolewa leo Machi 3,2023 na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Chongolo baada ya wananchi kutoa malalamiko kwenye kikao cha Balozi shina namba 2 katika kata ya Mtinko, kuhusu upatikanaji wa mbolea ambao umekuwa na changamoto nyingi katika kuipata.

Chongolo aliyekuwa anazungumza na Wana CCM na wananchi wa kata hiyo katika Kijiji cha Mtinko wilayani Singida amepokea malalamiko kuhusu mbolea ya ruzuku wanaipata kwa kupanga foleni na wakati mwingine baadhi yao hawana taarifa ya ujio wake na kutokana na umbali wa mbolea ilipo iwafikie wanatumia Sh.100,000 kwa mfuko mmoja kuifikisha walipo.

Baada ya maelezo ya wananchi pamoja na malalamiko yao kuhusu upatikanaji wa mbolea , Chongolo ametumia nafasi hiyo kuiagiza

Wizara ya kilimo kuhakikisha wanaongeza mawakala wa mbolea ili wakulima wengi waipate kwa urahisi na kwa wakati.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments