CCM yamtwika zigo la miradi DED Buchosa

            

Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza imemtwika zigo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa, Mwita Waryoba kuhakisha anakamlisha miradi ya maendeleo iliyokwama.

Kauli hiyo imetolewa na wajumbe wa kamati ya siasa CCM Machi 13, 2023 kwenye ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa laini ya CCM kwenye Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

Miongoni mwa Miradi hiyo ni ujenzi wa kituo cha afya Nyanzenda kilichotolewa fedha na Serikali kiasi cha Sh250 milioni ujenzi wake bado haujakilika na kuacha wakazi wa kata hiyo kukoswa huduma ya afya wakati Serikali imetoa fedha za mradi huo.


Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Marco Makoye amesikitishwa na watendaji wazembe wanaoshindwa kusimamia miladi ya maendeleo na kushindwa kukamilika.

"Tumefika mala kadhaa kwenye mradi huu nakutoa maelezo lakini hayatekelezwi jambo hilo halivukili tunapaswa kuchukuwa hatua,” amesema Makoye.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kituo cha afya Nyehunge, Martin Herman amesema chanzo cha kituo hicho kutokukamilika ni kutokushirikishwa kamati zilizoundwa za kusimamia mradi huo.

Amesema walipokuwa maofisa manunuzi wa Halmashauri ya Buchosa walijimilikisha kamati nyeti ya manunuzi na kuzinyima kamati haki kamati zilizoteuliwa na wananchi kusimamia mradi huo.

"Mambo yote yalikuwa yanafanywa na maofisa ununuzi na kamati zetu tulikuwa kama pambo tu, hivyo sisi tukasusia ndiyo hali iliyotufikisha sasa,” amesema Herman.

Kituo cha afya Nyanzenda ambacho ujenzi wake unasuasua nimiongoni mwa vituo vitatu vya afya vilivyotolewa na fedha na Serikali Kikiwemo Kituo cha afya Maisome sambamba na kituo cha afya Lushamba ambavyo viko hatua ya ukamilishaji.

Utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha afya Nyanzenda ulianza kutekeleza Novemba 11, 2021 na ujenzi huo ulipangwa kukamilika Mei 2022 lakini hadi sasa hauja kamilika.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa Mwita Waryoba amesema ana mwezi moja tangu amehamishiwa hapo na baada ya kuona ujenzi wa kituo hicho cha afya umekwama ameshatenga Sh40milioni kutoka mapato ya ndani.

"Nimepokea maelekezo ya kamati ya siasa nitatekeleza jukumu langu nikusimamia Mapato ya Halmashauri ili yakatekeleze miradi ya maendeleo,” amesema Waryoba.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments