Chongolo afoka Kiteto, ataka viongozi kuwa suluhisho la matatizo ya wananchi


 Serikali ina wataalamu na Wizara zilizoundwa kushughulika na masuala ya kisekta lakini kila kukicha wananchi wanahangaika kutaka kutafutiwa suluhisho la matatulizo yao bila mafanikio.

Hatuwezi kuwa nchi ya namna hiyo lazima tuwe watu wa kuhangaika kutafuta muda wa kutosha kwa wananchi kufanya shughuli zao na sio kuhangaika na changamoto.

Akizungumza na wananchi wa mji wa Kibaya Alhamisi Machi 9, 2023 mjini Kibaya kwenye mkutano wa hadhara, Katibu Mkuu wa CCM Taifa amesema ataenda kumuuliza Waziri wa Ardhi kuwa anafanya nini kuhakikisha anatatua migogoro ya ardhi sio tu Kiteto bali nchi nzima kwa kuwa kila kukicha kuna malalamiko ya wananchi kata kwa kata, wilaya na hata mikoa.


"Hatuwezi kugombania maeneo tu ya mipaka ya Kijografia, mpaka ambao mwananchi ukiamua kwenda wilaya nyingine huzuiwi wala kukatazwa kuishi wala kununua ardhi ya kujenga, sasa mipaka inatugombanishaje,"alisema Chongolo.

Alisema lakima kutakuwa na jambo...kuna viongozi ambao wanapewa bajeti ya Serikali lakini hawashuki chini kuja kutatua matatizo ya wananchi na kuyamaliza maana yake kuna ambao hawatimizi wajibu wao..hiyo ndio kazi yangu tutanyanyuana huko watuambie kwanini wananchi wanalalamika mwaka wa kwanza wapili watatu na wao wapo hayalimalizi tatizo nini, lazima tuwe wakali wakati mwingine alisema Chongolo

Alisema tukicheka  na nyani matokeo yake ni kuvuna mabua na sisi hatuwezi kukubali kuvuna mabua, lazima tuhangaike na mambo ya watu kwa sababu ndio yaliyotupa dhamana, ndio yaliyotupa heshima hii ndio yaliyomfanya ninyi wananchi mkusanyike kutusikiliza hapa, tusingekuwa na dhamana hii msigekuja hapa alisema Chongolo.

Alisema CCM haiwezi kuja kwa wananchi kuwapa matumaini yanayo eleaelea juu huo sio uongozi na mimi siko tayari kuwa kiongozi wa namna hiyo alisisitiza Chongolo.


Kuhusu suala la miundombinu na taa za barabarani aliwahakikishia wananchi wa mji wa Kibaya kuwa ifikapo mwezi wa sita taa ziwe zimewaka ili wananchi waweze kufanya kazi za kiuchumi wakati wote ili mradi wasivunje sheria na taratibu za nchi hii.

Kuhusu elimu Katibu Mkuu huyo amesema CCM imeielekeza Serikali kutafuta fedha wanakojua ili wanafunzi waweze kuanzishiwa shule za kidato cha tano na sita bure kuliko kujiendeleza kwenye vyuo vya kati na wengi kwenda shule binafsi.

"Tumeielekeza Serikali kwa kipindi cha miezi hii minne iliyobakia ambacho mwaka huu mwezi wa saba wanafunzi wanatakiwa kuanza kuripoti kidato cha tano na sita, Serikaki itafute hela inakojua kwa udi na uvumba ifikapo mwezi wa nne ipeleke fedha shule zinazofaa kuwa na kidato cha tano na sita ili kupanua wigo wa kupokea wanafunzi hao kwa mwaka huu na sio mwakani," alisisitiza Chongolo.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments