DKT.KIRUSWA,SERIKALI HAIKOTAYARI KUWAPOKEA WAWEKEZAJI AMBAO HAWATAKI KUINGIA UBIA.

Naibu waziri wa madini Dkt. Steven Kiruswa amesema serikali haikotayari kuwapokea wawekezaji ambao hawataki kuingia ubia katika sekta ya madini kwa sababu ni takwa la kisheria lililowekwa ili kunufaisha wazawa.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa jukwaa la pili la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya madini lililofanyika jijini Arusha.

"Wawekezaji ambao hawataki sera ya ubia na wanataka waendeshe mambo yao wenyewe kwa kweli ni bora waende kwa sababu hatuwezi kuwa na rasilimali za madini ambazo wananufaika wageni kutoka nje na si wazawa" amesema Dkt. KIRUSWA

Mbali na hilo waziri huyo akawaasa wale wote waliopata dhamana kwenye sekta hiyo ikiwemo wamiliki wa kampuni kufuata sheria ili serikali iweze kupata mapato kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Kwa upende wake kamishna wa madini Dkt.Abdulrahman Mwanga amesema wanachokifanya ni kuhakikisha wanawezesha wananchi ili kufanya biashara ya madini.

"Sekta ya madini kazi yetu ni kurahisishia wawekezaji na wafanyabiashara kufanyakazi zao vizuri ili waendelee kulipa kodi lakini pia kuhakikisha ushirikishwaji wa wananchi" amesema Dkt.Mwanga.

Naye Janeth Ruben Mwenyekiti wa kamati ya ushirikishwaji watanzania kwenye sekta ya madini amesema tangu sera na sheria ya ushirikishwaji ianze kutekelezwa imewezesha kuongezeka kwa idadi ya watanzania walioichukulia kama fursa sekta hiyo.

Naye mwakilishi wa wadhamini wakuu wa jukwaa hilo balozi mstaafu Ami Mpungwe ambaye ni mwenyekiti wa kampuni ya CMS ameeleza kuwa bado swala la ushirikishwaji wa wananchi kwenye sekta mbalimbali ni mdogo na jitihada zaidi zinahitajika na ndio hasa lililomsukuma kufadhili jukwa hilo.

Hata hivyo jukwaa hilo linalofanyika kwa muda wa siku tatu, linafanya pia maonyesho ya bidhaa mbalimbali zitokanazo na madini lakini pia kampuni za vifaa vinavyotumika kwenye uzalishaji.

Na Pamela Mollel. Arusha

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments