Hospitali ya Bugando yazindua tawi mjini Mwanza

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando (BMC) imefungua tawi jipya mjini Mwanza litakalotoa huduma za kitabibu za kibingwa kwa wagonjwa wa nje (OPD) kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali Kuu.

Pamoja na matibabu ya kawaida, tawi hilo lililofunguliwa eneo la Nera Barabara ya Makongoro pia itatoa huduma ya haraka kwa wagonjwa wenye mahitaji maalum watakaoweka miahadi na kuhudumia kwa wakati na muda wanaohitaji kwa malipo maalum.

Akizungumza leo Machi 4, 2023 wakati wa hafla ya uzinduzi wa kliniki hiyo iliyogharimu zaidi ya Sh2 bilioni, Mkurugenzi Mkuu wa BMC, Dk Fabian Massaga amesema tawi hilo linaweza kuhudumia wagonjwa wan je 500 kwa siku, na hivyo kupunguza msongamano kwa Hospitali Kuu ambayo kwa sasa inahudumia wagonjwa wan je zaidi ya 800 kwa siku.


Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi BMC, Askofu Renatus Nkwande amesema tawi hilo litahudumia wagonjwa kutoka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa inayojumuisha Mwanza, Mara, Simiyu, Kagera, Geita na Shinyanga. Hospitali ya Bugando pia inahudumia wagonjwa kutoka mikoa ya Tabora na Kigoma.

"Kutokana na ongezeko la wagonjwa, Hospitali ya Bugando imeimarisha hutoaji wa huduma kwa kuwafuata wananchi hadi vijijini kwa kununua mabasi mawili yatakayosafirisha madaktari bingwa na wataalam kwenda kutoa huduma vijijini,” amesema Askofu Nkwande

Mabasi hayo mawili aina ya Yutong yenye thamani ya zaidi ya Sh500 milioni pia yamezinduliwa tayari kuanza kuwasafirisha madaktari bingwa kwenda na kurudi vijijini kutoa kwa wananchi.

Charles Nyamasiriri, Diwani wa Kata ya Isamilo iliko tawi hilo jipya ameupongeza uongozi wa BMC kwa kusogeza huduma kwa wananchi huku akiomba huduma zitakazotolewa zilizngane na zile zinazotolewa katika hospitali kuu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments