Malawi yafunga shule kukwepa Kimbunga Freddy

Mamlaka ya elimu nchini Malawi imezifunga shule katika wilaya 10 kutokana na wasiwasi wa usalama baada ya Kimbunga Freddy kusababisha uharibifu katika nchi jirani ya Msumbiji.

Kwa mujibu wa BBC, mvua kubwa inayonyesha kusini mwa Malawi imeharibu barabara na kusitisha uzalishaji wa umeme, huku mvua zaidi zikitarajiwa kunyesha katika siku chache zijazo.

Masomo yamesimamishwa kuanzia leo Machi 13, 2023 Jumatatu na Jumanne katika taasisi zote za masomo katika eneo hilo.


Wizara ya Elimu nchini humo imeelekeza kwamba walimu na wanafunzi watumie majukwaa yanayopatikana mtandaoni na masomo ya redioni katika kipindi ambacho shule zimefungwa.

 “Wakati madarasa yatakaporejea walimu wanahimizwa kuongeza muda wa masomo ili kufidia muda uliopotea,” iliongeza.

Nchi jirani ya Msumbiji imepokea mvua ya zaidi ya mwaka mmoja katika wiki nne zilizopita, huku Kimbunga Freddy kikitua Jumapili kwa mara ya pili katika mwezi mmoja.

Idadi ya vifo nchini Msumbiji ni imefikia 28 tangu dhoruba hiyo ilikumbe taifa hilo kwa mara ya kwanza.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments