Mlata Awataka Wanachi Kusaidia Serikali Kufichua Wanaofanya Mauaji Manyoni










Mwenyekiti  wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Singida Martha Mlata amewataka wanachama na wananchi wa Manyoni kutoa ushirikiano kwa serikali katika zoezi la kubaini watu wanaohusika na mauaji ya watu wilayani Manyoni mkoani Singida.

Mlata amesema hayo  Machi 15, 2023 wakati akizungumza na wanachama wa CCM Wilayani humo ambapo amewataka  wanachama  wa CCM na wananchi wa Manyoni kwa ujumla kuwa wa kweli kwa kutoa taarifa za ushaidi kwa serikali wakati wa kubaini watu wanaohusika na mauaji yanayotishia amani Wilayani Humo.

"Tulimwita Mkuu wa mkoa na kazi imeanza, ukija kuulizwa kama unajua jambo usikatae Sema ukweli  kuisaidia serikali na kama unashindwa funga safari kwa Mkuu wa Mkoa ukamwambie muitonye serikali, naomba mtulie na Waziri wa Mambo ya Ndani alikuja kwahiyo haya mambo yanaendelea kufanyiwa kazi na wakianza kukamatwa msiwape dhamana." Alisema Mlata.

Aidha ameongeza kwa kuwataka wananchi hao  kutumia chama cha Mapinduzi Kuwasilisha kero zao ili zitatuliwe kwa haraka kwa kuwa chama hicho kipo kwaajili ya kuwahudumia watu hasa pale inapojitokeza changamoto.

"Ukitaka changamoto zako zitatuliwe kwa haraka leta kwenye Chama, kwahiyo kero zote tuzifikishe kwenye chama ili chama kitapeleka  serikalini tuna Madiwani, Wabunge, Watendaji wa Vijiji na kata, Wenyeviti wa halmashauri, tuna Wakurugenzi, Mkurugenzi akiitwa na Mwenyekiti wa Chama atatekeleza" Alisema Mlata.

Naye MNEC Mkoa wa Singida Yohana Msita Amewahimiza wananchi wa Manyoni kuungana kuwa kitu Kimoja katika kupambana na watu wanaotaka kuirudisha Manyoni nyuma ili kuchochea Maendeleo katika nyanja Mbalimbali.

Msita alisema kuna watu bado wanachochea watu kutengena na kugawanyika jambo ambali alilikataa na kuwataka wananchi kuwa pamoja katika kuzikabili changamoto za namna ile.

"Wanamanyoni Lazima tuunganie tuwe kitu Kimoja asiwepo mtu wakutupasua,watukugawa huyo atatuchelewesha kwenye maendeleo wapo baadhi ya watu hawatutakii mema wanatamani watuone tumegawanyika tumepalanganyika ili yasiwepo maendeleo lakini sisi Watu wa Manyoni tunatakiwa kupinga kwa nguvu Kubwaa, tumuone kuwa ni adui mkubwa mtu anayetugawa anayetupalaganyisha ule umoja, upendo tuudumishe." Alisema Msita.

Awali Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilayani humo Jumanne Ismail alizitaja changamoto ambazo zimekuwa kero kwa wananchi jambo ambalo linawapa wakati mgumu pindi wanapo kutana nao.

Alizitaja changamoto hizo kuwa in Pamoja na kukithiri kwa mauji ya watu ambapo chama hicho kimeendelea kulaani, jambo jingine ni kukatika kwa Umeme hali inayokwamisha shuguli nyingi za uzalishaji jambo alilolitaja kuwa changamoto hiyo inakipunguzia chama cha Mapinduzi kura kwa wanachama wake.

Aidha suala lingine ambalo bado ni kitendawili ni kutokuwepo kwa usawa kwenye ugawaji wa Mahindi ya ruzuku ya serikali ambapo baadhi ya kata hazijapata Mahindi mpaka sasa akitolea mfano kata Rungwa iliyompakani mwa Singida na Mkoa wa Mbeya.

Na Hamis Hussein – Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments