MWANAMKE NA UCHUMI SINGIDA INAWEZEKANA

                   
Iwapo wanawake watajikita kwenye shughuli za ujasilimali na kujiendeleza kitaaluma kutasaidia kupunguza vitendo vya ukatili dhidi yao kutoka kwa wanaume wenye silika hiyo na hatimaye kujenga jamii bora.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano Machi 8, 2023 na Meya Wa Manispaa Singida  Bi Yagi Kiaratu   wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Katika Uwanja Wa bombadia Zamani (Peoples) Manispaa Ya Singida

"Mwanamke ni kiunganishi kikuu ndani ya familia, hivyo hatakiwi kuyumba katika nyanja za kiuchumi na kielimu na hata malezi akiyumba atakuwa ameyumbisha familia na jamii," amesema  Yagi Kiaratu


Amesema kuwa hata akiwa mwajiriwa kwenye taasisi ya umma au hata binafsi suala la ujasiriamali hatakiwi kulikwepa kulingana na uchumi wa sasa kwani bila kufanya hivyo atakuwa anajirudisha nyuma.

Kwa upande wake Mwenyekiti Wa CCM Manispaa Ya Singida Bi Lucia Mwilu    amesema kuwa wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Wanawake kwenye mataifa mbalimbali wanawake wanapaswa kuendeleza ujasiri wao wa kupambana na vitendo vya ukatili vinavyochangia kurudisha nyuma maendeleo.

Aidha Bi Lucia Mwilu  ameitaka jamii kutorudi nyuma katika kushirikiana na Serikali kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ili kujenga Taifa bora na imara.

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo  Yaliyofanyika Manispaa Ya Singida Alikuwa Meya Wa Manispaa Hiyo  Bi Yangi Kiaratu   amewataka wanawake wenye dhamana mbalimbali Katika Manispaa hiyo  kuzitumia vizuri ili kulinda jamii katika nyanja mbalimbali.


Post a Comment

0 Comments