Odinga amkalia kooni rais Ruto


 Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema hatasitisha maandamano ya nchi nzima aliyopanga kufanya Jumatatu na wafuasi wake.

Kwa mujibu wa kituo cha habari ‘The EastAfrican’ leo Machi 17,2023 Odinga aliyehutubia katika Jiji la Nakuru jana alisema maandamano hayo yatakuwa ya Amani na wala hatishiki na vitisho vya Rais wa nchi hiyo William Ruto na maafisa wengine wa serikali.

“Nataka kuwaambia kwamba nilipigania ukombozi wa pili katika nchi hii, wawili hao hawawezi kuelewa nilichopitia. Nilikamatwa, nikashtakiwa mahakamani na kwenda jela mwaka 1983 lakini nikaachiliwa kwa kukosa ushahidi,” Odinga amesema.

“Nimekuwa nikipigania demokrasia na nimewekwa kizuizini kwa miaka minane wakati baadhi yao walikuwa bado wananyonyesha. Simba (Rais wa amani wa Kenya Daniel Arap Moi) aliogopwa lakini tuling’oa meno yake.Nimejitayarisha kulipa gharama kubwa nikipigania ukombozi wa Kenya.”

Wakati huo huo, Kalonzo Musyoka, kiongozi wa chama cha Wiper alisema maandamano hayo yatakuwa ya amani, akionya mataifa ya kigeni dhidi ya kuingilia masuala ya Kenya. 

“Maandamano yetu yatakuwa ya amani na hayatamlenga mtu yeyote. Yeyote atakayeleta vurugu si sehemu yetu. Tutaandamana hadi William Ruto aondoke Ikulu,” alisema Musyoka.

"Tunajua wana mipango ya kutumia wafuasi wao wachache kupora maduka na kulaumu Azimio (muungano wa upinzani), lakini tutakuwa na nidhamu kubwa. Katiba inatupa uhuru wa kutosha.”
 

Imeandaliwa na Emmanuel Msabaha kwa msaada wa mashirika.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments