Rais Samia amteua Pinda kuongoza baraza la kumshauri kilimo


 Rais Samia Suluhu Hassan ameunda Baraza la kumshauri kuhusu utekelezaji wa masuala ya kilimo na chakula litakaloongozwa na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda.

Pinda ambaye ndiye Mwenyekiti atawaongoza wajumbe wawili na baraza hilo na wengine watatu watakaounda sekretarieti.

Uteuzi wa Pinda kushika wadhifa huo umetangazwa leo, Machi 14, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.


Mbali na Pinda, wengine walioteuliwa na Rais Samia katika baraza hilo ni Geoffrey Kalenga mkurugenzi mtendaji wa SAGCOT na Andrew Massawe watakaokuwa wajumbe.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wajumbe wa sekretarieti ya baraza hilo ni Dk Florence Turuka mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Dk Jacqueline Mkindi mkurugenzi mtendaji Chama cha Wakulima wa Mbogamboga na Matunda Tanzania (TAHA) na Dk Mwatima Juma Mwenyekiti wa Taasisi ya Kuendeleza Kilimo Hai Tanzania (TOAM).

Kuundwa kwa baraza hilo ni matokeo ya mkutano wa utoshelevu na ustahimilivu wa chakula uliofanyika Dakar nchini Senegal.

Katika mkutano huo uliofanyika Februari 25 hadi 27, mwaka huu na kukutanisha wakuu wa nchi za Afrika, waliazimia kila nchi kuunda baraza la kusimamia utekelezaji wa mikakati ya kukuza kilimo na kuongeza uzalishaji wa chakula.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments