Rais Samia mgeni rasmi mkutano wa Bawacha

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ulioandaliwa na Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha) itakayofanyika Machi 8 mwaka huu mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Machi 5, 2023 Mbowe amesema kuridhia kwa Rais Samia kumetokana na mwaliko waliompa siku chache zilizopita.

“Nikitambua namna ambavyo tumefanya kazi na Rais Samia tumekubali tumualike naye amekubali kuhudhuria aje awasikie wakinamama wa Chadema, kina mama wa upinzani.


“Siku zote anawasikiliza wakina mama wa chama chake, aje awaone atambue kazi kubwa inayofanywa na akina mama wa Chadema kwa hiyo Rais atakuwa mgeni rasmi katika tukio letu na mimi nitakuwepo kumpokea,” amesema Mbowe.

Amesema katika mkutano huo si Rais Samia pekee, wanawake wenye itikadi mbalimbali za kisiasa wamealikwa kwa kile alichokifafanua kuwa maadhimisho hayo si ya Chadema bali ya wanawake wote duniani.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments