Waliovamia Msitu Wa Ngimu Kuondolewa Baada Ya Mavuno- Rc Serukamba

MKUU wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba  amemueleza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) pamoja na wananchi wa Kijiji  Cha Ngimu mkoani  Singida kwamba watu wote waliovamia msitu wa Ngimu wataondolewa baada ya msimu wa kilimo kumalizika kwani kuna baadhi yao wamelima na wengine kujenga.

Serukamba ametoa kauli hiyo mbele ya Chongolo baada ya kutakiwa kutoa majibu kutokana na malalamiko ya baadhi ya wananchi kwamba licha ya jitihada za kuulinda msitu wa mgori lakini wapo baadhi ya watu wamevamia na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji,Hali inayosababisha kuuharibu hifadhi ya msitu huo.
 wa Mgori.

Akielezea zaidi Mkuu wa Mkoa huyo amesema kwamba ni kweli Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) wameweka alama za lakini alikuta tayari kuna maamuzi ya Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa,wakati wanasubiri kipindi cha mvua kipite na wanasubiri kwasababu moja wanajua watu wamelima kwenye msitu.

"Tukasema sio sahihi kwenda kuwaondoa mazao yao , nataka nitumie nafasi hii kuwaaambia ule msitu lazima tuulinde tumeamua tusubiri mmalize kuvuna tukija mtutajie watu wote waliolima ndani ya msitu tutawaondoa

"Kuna mzee mmoja pale ameuliza swali la msingi,amesema Kuna msitu wanaopeleka ng'ombe,Kuna wanaolima nani anaharibu msitu zaidi wote wawili wanaharibu msitu wetu, nami niwaambieni ndugu zangu ni muumini wa kulinda misitu ,kwa hiyo nimeamua tuache wale mliolima najua mko hapa tusiwanyang'anye mazao yenu.

"Lakini nitakuja na Kamati ya Ulinzi na Usalama watu wote waliolima kwenye msitu wa pori ,wanaoishi kwenye msitu wa pori tutawaondoa ,tukishamaliza kuwaondoa tutawaomba TFS walete ulinzi wao kulinda baada ya sisi kuwa tumesafisha,"amesema Serukamba.

Awali mmoja ya wananchi wa Kijiji hicho alimueleza Katibu Mkuu CCM kwamba kwenye Kijiji chao kuna mradi wa pori ambao umekuwa ni kero kwani Wananchi walijitoa kwa ajili yao ili walinde hifadhi  lakini sasa hivi limevamiwa

"Sasa tatizo hili limekuwa ni wimbo wa  muda mrefu sana kwa hiyo naomba Serikali yako kwasababu usimamizi umekuwa ni mgumu , uchukue hili suala uone huu mzigo utakavyofanya ndugu Katibu Mkuu."


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments