Zitto asema hawakati tamaa, kupigania haki ya wananchi

Kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema chama hicho hakitakata tamaa na  kitaendelea kupigania haki za wananchi ikiwemo kuchagua viongozi wanaowataka kuwaongoza.

Mbali na hilo, Zitto amesema watahakikisha wanaendelea kusemea pia changamoto zinazowakabili wananchi ili kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi na kutoa mawazo mbadala kwa Serikali kupitia baraza kivuli la chama hicho.

Ametoa kauli hiyo, leo Jumapili Machi 12, 2023 wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Baraza la Eid wilayani Tunduru mkoani Ruvuma. Mkutano huo ni mwendelezo wa ziara ya kuimarisha chama hicho, iliyowahusisha viongozi wakuu.


Zitto amesema ndio maana ya uchaguzi mkuu mwaka 2020 kumalizika na CCM kunyakua viti vya udiwani na ubunge, ACT- Wazalendo kiliendelea  kusema changamoto mbalimbali za Watanzania pamoja na kudai demokrasia  mazingira ya siasa kuwa mazuri.

" Ndio maana tuliamua kuunda baraza la mawaziri kivuli ili kusemea changamoto za wananchi na kutoa mawazo mbadala kwa Serikali.

"Tulikuwa na machaguo tuendeleea na mapambano au tupambane ndani ya nchi, lakini tukasema hatuwezi kukimbiia changamoto zilizojitokeza.

Zitto ambaye ni mbunge wa zamani wa Kigoma Kaskazini, amesema baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu 2020 alifuatwa na balozi tatu zilizompa ofa ya kuondoka kutoka mazingira kutokuwa rafiki baada ya mchakato huo kumalizika.

"Lakini nikawaambia siwezi kuondoka...Sisemi  hivi kudogosha waliokimbia nje ya  bali katika mapambano kuna njia nyingi za kukabiliana na  tatizo," amesema Zitto.

Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo, Ado Shaibu amewataka wananchi Tunduru kuendeleza  mshikamano na mapambano, licha ya kutochaguliwa kuwa mbunge wa Kaskazini atahakikisha anabeba hoja na ajenda zinazowakabili wananchi wa majimbo ya Tunduru Kaskizini na Kusini.


Katika mkutano huo, Shaibu pia aligusia suala la uvamizi wa tembo katika makazi ya watu, akiitaka Serikali kufanya utafiti wa kubaini sababu za wanyama hao kutoka mbugani kwenda katika vijiji na kuleta madhara kwa wananchi wanaoishi maeneo hayo.

Waziri Kivuli wa Kilimo, Abdallah Mtutura wa ACT- Wazalendo, alisema suala la wakulima kujiorodhesha kwa ajili ya kupata mbolea sio mzuri, akisema unawaletea usumbufu mkubwa kwa wananchi hasa wakulima wa maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments