Recent-Post

Ajali yaua Mwandishi wa habari Iringa

Mwandishi wa habari mwandamizi wa Kituo cha Televisheni cha Iringa (IMTV), Rashid Msigwa (38) amefariki dunia baada ya kupata ajali ya gari katika barabara kuu ya Tanzania-Zambia eneo la Ipogolo Manispaa ya Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatano Aprili 19, 2023 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa ACP, Allan Bukumbi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo usiku wa kuamkia jana.

Bukumbi amesema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Subaru Impreza iliyokuwa ikitokea Kitwiru kuelekea Ipogolo Manispaa ya Iringa iliyogonga pikipiki kisha kuhama njia na kwenda kugonga mti.


Post a Comment

0 Comments