CCM yawanyoshea vidole makada wanaotengeneza makundi, migogoro Zanzibar


 Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM, Zanzibar, Khamis Mbeto amemesema chama hicho hakitawavumilia baadhi ya viongozi na wanachama wanaoendeleza makundi ya kuwagawa wanachama na kutengeneza migogoro majimboni.

Mbeto ametoa kauli hiyo leo Aprili 20, 2023 wakati wa hafla ya kugawa vyakula kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitr kwa wanachama na wananchi wa Jimbo la Pangawe, Unguja.

Amesema chama hakitaona shida kurudia uchaguzi wa viongozi wa jimbo lolote Zanzibar endapo kitabaini kuna baadhi ya viongozi wanaotumia nafasi zao kukumbatia makundi yanayotengeneza migogoro na fitna ndani ya jimbo hilo.


“Haya makundi yanatakiwa kuvunjwa kila unapoisha uchaguzi na kupigania maslahi ya chama, lakini wapo watu bado wanaendeleza makundi hayo na fitna, chama hakitaona muhali kurudia uchaguzi ka kingozi atakayebainika kukengeuka,” alisema Mbeto

Mbeto, amesema wanaofanya hivyo ni usaliti kwani madhara yake yanasababisha kudumaza kasi za utendaji za viongozi waliopo madarakani kwa sasa.

Alitaka viongozi waliopo madaraka wapewe nafasi ya kuwatumikia wananchi na itakapofika wakati wa kuwania nafasi hizo kila mwanachama atakuwa na haki ya kuombea na atapendekezwa na chama kwa mujibu wa sifa na vigezo alivyonavyo.

"Natoa angalizo kwa yeyote anayeendeleza makundi ya kujipitisha majimboni kufanya fitna na migogoro ajue kuwa taarifa zake tutazipata na wakati ukifika hatoweza kuvuka salama,” amesema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa jimbo hilo, Ali Suleiman Ameir, amesema lengo la sadaka hiyo ni kuirejesha shukrani kubwa kwa wananchi kutokana na juhudi zao za kuimarisha umoja na mshikamano.

Naye Mwenyekiti wa jimbo hilo Dadi Juma Dadi, amesema jimbo hilo lipo salama kisiasa, kiuchumi na kijamii licha ya kukabiliwa na changamoto ya baadhi ya makada kujitokeza kutangaza nia za kugombea nafasi mbalimbali jimboni humo kabla ya wakati wa uchaguzi uliopangwa kikatiba.

Sadaka hiyo ya mchele na tende vimegawiwa kwa makundi matatu ya wananchi ambao ni wazee, watu wasiojiweza na wanachama na wananchi wa jimbo la Pangawe ambapo wamepokea mchele na tende.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments