Recent-Post

Daraja la kuunganisha Zanzibar, Tanzanzia Bara mbioni kujengwa

Serikali imeanza mazungumzo kuhusu ujenzi wa daraja litakalounganisha Tanzania Bara na Zanzibar ili kurahisisha usafiri kwa pande zote mbili.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Ijumaa Aprili 28, 2023 na Naibu Waziri wa Ujenzi na uchukuzi, Geofrey Kasekenya ambaye amesema mazungumzo hayo yalifanyika Machi 11, 2023.

Naibu Waziri alikuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Mwantumu (CCM), Dau Haji ambaye ameuliza Serikali ina mpango gani wa kujenga daraja linalounganisha Tanzania Bara na Zanzibar.



Post a Comment

0 Comments