Dk Mpango: Waumini ombeeni viongozi wa Serikali

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Mpango ametoa wito kwa waumini na viongozi wa dini nchini kuendelea kuwaombea viongozi wa Serikali ili waongoze nchi kadri ya mapenzi ya Mungu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais imesema Dk Mpango ameyasema hayo leo Jumapili Aprili 23, 2023 wakati akiwasalimu waumini mara baada ya ibada ya Jumapili iliofanyika katika Nyumba ya Malezi ya Mtakatifu Yosefu iliopo Miyuji Jimbo kuu katoliki Dodoma.

Ibada hiyo ilioongozwa na Padre Stanslaus Mitti, Mpango amesema ni vema kuendelea kuiombea nchi iwe na amani wakati wote pamoja na viongozi na watumishi wa Taifa waweze kutenda kazi kwa hekima ya Mungu.

Vilevile amewakumbusha waumini na Watanzania kwa ujumla umuhimu wa malezi kwa watoto na vijana kuanzia nyumbani.Amesema ni vema wazazi wakafanya kazi ya ziada katika kufuatilia mienendo ya watoto na vijana, wakike kwa wakiume mahali popote ikiwemo vyuoni.

Halikadhalika, ametoa wito kwa waumini wa kanisa hilo na wananchi wa Dodoma kuongeza jitihada katika usafi wa mazingira, kupanda miti na maua na kuepukana na tabia za kutupa taka ovyo katika maeneo yao.Amesema Mwenyezi Mungu ameijaalia Tanzania mazingira mazuri hivyo hakuna budi kuitunza kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments