Halmashauli Kuu Ya Wilaya Ya Ikungi Yatekeleza Kwa Vitendo Katika Miradi Mbali Mbali Wilayani Humo.

                  

Halmashauri kuu ya wilaya Ikungi ikiongozwa na mwenyekiti wake Bw. Mika Likapakapa imepokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM iliowasilishwa na mkuu wa wilaya ya Ikungi Bw. Thomson Apson.

Katika uwasilishaji wake  Mkuu wa wilaya ya Ikungu Bw.Apson amemshukuru sana Mh Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi za miradi katika wilaya ya Ikungi.
Miradi ambao iliotekelezwa kwa kiwango kikubwa ni miundo mbinu ya maji, barabara,umeme ,afya na shule. 

Aidha  mkuu wa wilaya Bw. Apson, amewajulisha wajumbe kuwa kuanzia wiki ijayo kutakuwa na ujenzi wa shule mpya tatu ambao ni shule ya sekondari moja itakayojengwa katika kata ya Iyumbu,shule ya msingi Ituru katika kata ya Makilawa na shule ya msingi Tambuka reli ilioko katika kata ya Ikungi. 

Wajumbe kwa ujumla wao walimpongeza sana  Mkuu wa wilaya kwa taarifa yake na kumshauri baadhi ya mambo Kwajili manuafaa mbali mbali katika jamii na taifa kwa kwa ujmla.

Pia wajumbe walimpongeza sana mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi ndugu Justice Kijazi na wataalamu wake kwa kufanya kazi kwa bidii na kupelekea  halmashauri ya wilaya kupata hati safi.

Wakielezea hati safi iliopatikana katika wilaya ya Ikungi,wajumbe pia waliwashukuru sana madiwani wakiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri ya Ikungi Mh Ally Juma Mwanga kwa usimamizi mzuri wa miradi na kupelekea,  miaka zaidi ya nane kupata hati safi.

Mwenyekiti wa halmashauri aliwashukuru sana waheshimiwa wabunge kwa kuendelea  kusaidia miradi mingi kuja katika wilaya ya Ikungi na kuendelea kutoa ushirikiano katika kuteleza mirada mbali mbali inayoendelea wilayanihumo
   
Hata hivyo wajumbe wa halmashauli kuu ya wilaya ya ikungu kwa pamoja waliiunga mkono taarifa hiyo.

Chanzo Na Ofisi Ya Mbunge 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments