‘Kila nchi majukumu yake yatambulike kwenye Muungano’

Wakati Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukisherekea miaka 59 tangu uasisiwe Aprili 26, 1964, imelezwa ni muhimu kuwa na Muungano imara wenye kutambua majukumu ya nchi zilizoungana.

Hayo yameelezwa Jana  Jumatano, April26, 2023 katika mjadala kwa njia ya mtandao wa Twitter Space uliopandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) ukiwa na mada ‘nini kifanyike ili muungano baina ya Tanzania bara na Zanzibar udumu’.

Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo mkoani Lindi, Isihaka Mchinjita amesema Muungano uliopo sasa unatoa ugumu hata kuelezewa kutokana na baadhi ya mambo kuwa katika kificho.


“Hatupaswi kuainisha changamoto zinazotishia Muungano wetu, bali kuweka msingi nzuri wa Muuungano wa Tanganyika na Zanzibar. Aina ya Muungano uliopo ni kama vile nchi moja imeimeza nyingine bila yenyewe kupenda.

Kuna umuhimu wa kupata Katiba Mpya, ni muhimu kuheshimu maoni ya Wazanzibari. Mazingira ya sasa ya Muungano yanazalisha upande kulalamika zaidi. Tufike mahali Muungano ambayo Watanganyika watakuwa na furaha kuungana na Wazanzibar na kila mmoja wetu atakuwa na uelewa kuhusu Muungano.

Amesema ni muhimu kuwepo kwa Muungano ambao kila nchi itakuwa na furaha kuuelezea na kunufaika kuliko Muungano uliopo sasa ambao umeimeza nchi moja.

Mchinjita amesema muundo Muungano uliopo unachangamoto nyingi na unaleta ukuaji mdogo wa maendeleo katika nchi, hivyo tufanyie mapitio muungano uliopo uonyeshe kuonyesha ni fursa zipi zinapaswa kuwa za muungano na zipi si za muungano.

Kwa upande wake, Waziri Kivuli wa Utumishi na Utawala Bora na Muunganowa ACT-Wazalendo, Pavu Abdallah amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar bado umekuwa na changamoto nyingi zinazosababisha upande mmoja kuona kama unapendelewa.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments