MADUKA SABA MABIGWA POLISI JAMII CUP 2023 SINGIDA

                  

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Stellah Mutahibirwa. akizungumza kwenye michuano hiyo, amesema mashindano hayo yana lengo la kupinga vitendo vya ukatili na matukio mengine ya uhalifu eneo hilo.

(ACP) Stellah Mutahibirwa. amesema kwa kupitia fursa ya Polisi Jamii itasaidia kuiweka jamii karibu na polisi, jambo litakalowezesha kupata taarifa za uhalifu kwa urahisi na kuwaondoa wananchi hofu iliyojengeka kwa polisi.

Amesema wameandaa mashindano hayo ikiwa ni utaratibu uliopo chini ya IGP Camillus Wambura lengo likiwa kutoa elimu juu ya tabia hatarishi na vijana kuwa na afya bora kupitia michezo hivyo kuwaepusha vijana kuacha tabia za matumizi ya dawa za kulevya, bangi na ulevi ambavyo huchangia kuzorotesha uchumi wa nchi.

Mwenyekiti wa chama cha soka  Mkoa Wa Singida (SIREFA ),Bw Hamisi Kitila  amewapongeza polisi kwa kuanzisha michuano hiyo ambayo itachangia vijana kushiriki michezo.

Maduka Saba wakisheherekea ubingwa kwa pamoja na Jeshi la polisi

Washindi Wa Tatu Timu Ya Minzani Fc wakiwa pamoja na Jeshi La Polisi

Waamuzi Wa Mchezo Wa Fainali ya Polisi Jamii Cup Singida Wakiwapamoja na jeshi la polisi

Picha Ya Kikosi Cha Maduka Saba(Bingwa)

                         Washindi Wa Pili Kwenye Mashindano Ya Polisi Jamii Cup .Msufini
Na Mwandishi Wetu Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments