MAANDALIZI YA LIGI YA MPIRA WA MIGUU WILAYA YA IRAMBA (IRAMBA SUPER CUP 2023)

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleimani Yusuph Mwenda amekabidhi jezi seti 29 kwa Viongozi wa Kata kumi za awamu ya pili ambao watazigawa katika Timu za vijiji husika vitakavyosbiriki kwenye mashindano ngazi ya Kata kwa ajili ya Maandalizi ya Ligi ya Wilaya ya Iramba (Iramba Super Cup 2023) inYotarajiwa kuanza Mwishoni mwa mwezi Mei .

Akipokea Jezi hizo kwa niaba ya Viongozi wa Kata hizo Diwani wa kata ya Shelui Mhe. Agnes Nassania amemshukuru sana Mkuu wa Wilaya ya Iramba kwa kutoa jezi hizo bazo zitasaidia kuwahamasisha vijaja kwenye vijiji hivyo kushiriki michezo kwani itasaidia kuinua vipaji na kujenga ushirikiano kwa Vijana hao

DC Mwenda amekamilisha kugawa jezi kwa Timu za vijiji 70 vilivyopo katika Wilaya ya Iramba ikiwa ni mkakati wa maandili za Ligi ya wilaya ya Iramba.

         

            

              
Chanzo dcirambaofficial

Post a Comment

0 Comments