Mafuriko yasababisha magari kusitisha safari barabara Arusha-Moshi


 Mvua zilizoanza kunyesha usiku wa kuamkia  leo Jumatatu, Aprili 3, 2023 katika maeneo mbalimbali mkoani Kilimanjaro imesababisha mafaruko na kusababisha kukatika kwa mawasiliano katika barabara kuu ya Moshi-Arusha  eneo la kwa Msomali Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro kwa zaidi ya saa tatu.

Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Simon Maigwa amekiri kutokea kwa adha hiyo na amesema maji hayo ni mengi na kwa sasa hakuna magari yanayoweza kupita kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.

"Ni kweli kwa sasa eneo la kwa Msomali halipitiki maji ni mengi kupita kiasi, magari yamesimama kwa muda na hayawezi kutoka upande wa Moshi  kwenda Arusha na upande wa Arusha kwenda kuja Moshi," amesema.

Kamanda Maigwa ambaye amesema yuko njiani kelekea eneo la tukio na amewataka wananchi na wasafiri kuwa na subira wakati huu ambapo jeshi hilo kwa kushirikiana na mamalaka nyingine ikiwemo Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) kutafuta ufumbuzi.

Meneja wa Tanroad mkoani hapa, Mota Kyando ameliambia gazeti hili kuwa wako eneo la tukio kutafuta suluhisho la tatizo hilo ili shughuli za usafiri ziweze kuendelea kama kawaida.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kilimanjaro (RSA), Khadili Shekoloa amesema yupo eneo hilo kushirikiana na mamlaka nyingine kuhakikisha usalama unakuwepo katika eneo hilo.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments