Mbunge wa Mtinga alia na makato ya viingilio timu za Tanzania

Mbunge wa Iramba Mashariki, Francis Mtinga (CCM) ameomba Serikali kufanya upya mapitio ya kodi zinazotozwa kutokana na mapato ya viingilio uwanjani ili kuzisaidia timu za Tanzania.

Mtinga ameliambia bunge leo Ijumaa Aprili 28, 2023 wakati akiuliza swali la nyongeza ambapo amesema viwango vinavyotozwa haviendani na uhalisia kwani kuna alichokiita kunyonywa.

Ametolea mfano wa mchezo wa Simba na Yanga uliochezwa hivi karibuni ambapo ilitangazwa kuwa zilikusanywa Sh450 milioni lakini cha kushangaza ni kuwa timu mwenyeji Simba ilipatiwa Sh180 milioni ambacho ni kiwango kidogo.


“Ni lini Serikali itaondoa tozo na makato hayo ili kuzisaidia timu zetu ziweze kujiimarisha kiuchumi badala ya kuwa na unyonge wa kiuchumi kila wakati,” amesema Mtinga.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, Hamis Mwinjuma amesema itakuwa vigumu kuondoa kodi hiyo kwani inasaidia katika uendeshaji wa shughuli za michezo.

Mwinjuma amesema suala la kuendesha timu ni gumu na kwamba viwango vinavyokatwa husaidia kufikisha malengo hayo licha ya kuwa Serikali inatamani kuona timu zikiendelea kuimarika.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments