Mkurugenzi Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali afa ajalini

Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Katiba na Sheria Dk Abdul Mussa, amefariki dunia jana Jumapili Aprili 23, 2023 saa sita mchana baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Dodoma kupata ajali eneo la Mdaula wilayani Bagamoyo.

Taarifa hiyo imethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Pius Lutumo amesema ajali hiyo baada ya gari aina ya Toyota Hilux alilokuwa akisafiria likiendeshwa na Alex Festo kuligonga kwa nyuma gari aina ya Howo lililokuwa linaendeshwa na Rashid Mohamed.

"Tunaendelea kuwashikilia madereva wote waliokuwa wanaendesha magari hayo na chanzo cha ajali bado tunaendelea kukichunguza,"amesema


Amesema kuwa mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani, Tumbi kusubiri taratibu nyingine.

Kamanda Lutumo amesema katika ajali hiyo hakuna majeruhi yoyote zaidi ya kifo cha mkurugenzi huyo na amewataka madereva kuongeza umakini pindi wawapo barabarani Ili kuepusha ajali zinazoepukika ambazo husababisha vifo, uharibifu wa mali na miundombinu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments