Rais atengua uteuzi wa Mkurugenzi Jiji la Mwanza

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Sekiete Yahaya Selemani kuanzia Aprili 16 mwaka huu.

Taarifa hiyo imetolea leo Jumanne, Aprili 18, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu kwa vyombo vya habari.

Hata hiyo imekuja zikiwa zimepita siku 96 tangu Januari 13, 2023, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima 'alimshitakii' mkurugenzi huyo kwa Wizara ya Nchi katika Ofisi ya Rais Tamisemi ambayo ndio mamlaka yake ya nidhamu, akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Sh1 bilioni.


Wakati barua ya mashtaka ikitua Tamisemi, Malima aliagiza watumishi wanne wa jiji hilo kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa tuhuma za uuzaji wa viwanja hivyo.

Akizungumza na vyombo vya habari, Malima aliwataja wanaosimamishwa kazi kwa nyadhifa zao kuwa ni mhasibu wa Jiji, mwanasheria, ofisa manunuzi na ofisa mipango.

Watumishi hao wa umma wanadaiwa kuuza viwanja hivyo vilivyopo mtaa wa kibiashara katikati ya jiji kwa thamani ndogo kulinganisha na bei ya soko.

Amesema walishirikiana kuuza viwanja hivyo bila kufuata utaratibu kinyume cha taratibu na maadili ya viongozi huku Mkurugenzi wa Jiji akidaiwa kukiuka maagizo ya kamati ya ulinzi Wilaya ya Nyamagana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

"Kwa mamlaka yangu nimeelekeza ofisi ya katibu tawala Mkoa wa Mwanza iwasimamishe kazi watumishi wanne ambao ni wakuu wa idara kupisha uchunguzi na tunaandika barua ofisi ya Rais (Tamisemi) kwa hatua kuhusu mkurugenzi wa Jiji," alisema Malima.

Mkuu huyo wa mkoa alisema licha ya suala la maamuzi kuachwa mikononi mwa Tamisemi, mamlaka ya mkoa iliona kuwa kiongozi huyo amekosa sifa za kuendelea kusalia mkoani humo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments