RAIS KAGAME AHITIMISHA ZIARA YA KIKAZI NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania na kurejea nchini Rwanda.

Mheshimiwa Kagame ameagwa katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) ambaye aliambatana na; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu – Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye.

Viongozi wengine waandamizi wa Serikali waliomsindikiza ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makala, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Balozi wa Rwanda Nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz.

Akiwa nchini Rais Kagame pamoja na mweyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan walikubaliana kuimarisha masuala mbalimbali ya ushirikiano hususan biashara, miundombinu ya bandari, mradi wa umeme wa Rusumo pamoja na masuala ya ulinzi na usalama.

 Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakati akiondoka kurejea nchini Rwanda

 Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akiagana na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kabla ya kurejea nchini Rwanda

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakimuaga Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam


  Ndege ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame na ujumbe wake ikiwa tayari kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kurejea nchini Rwanda

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments