Rais Samia atoa ujumbe wa Eid

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za Sikukuu ya Eid al-Fitr akiwataka waumini wa Kiislamu na Watanzania kusherekea kwa amani.

Waislamu wa Tanzania wanaungana na Mataifa mbalimbali duniani kusherekea sikukuu hiyo leo Jumamosi Aprili 22,2023.

Mkuu huyo wa nchi, ametumia ukurasa wake wa Twitter kutoa salamu hizo akisema,"nawatakia nyote kheri ya Sikukuu ya Eid al-Fitr."


"Kuandama kwa mwezi ni hitimisho la funga yetu lakini pia ni wakati wa kuendeleza misingi tuliyoishi katika siku hizi 30; misingi ya kutenda yaliyo mema, kuwajali wengine, sadaka, shukrani na ibada kwa Mwenyezi Mungu. Eid Mubarak."

Katika hatua nyingine, Rais Samia ameswali sala ya Eid leo Jumamosi, katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI Bakwata Makao Makuu, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments