Rais Samia awateua Diamond, Shilole Baraza la Malaria

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameteua Baraza la kutokomeza Malaria nchini lenye wajumbe mbalimbali wakiwamo mawaziri, wanamichezo, viongozi wa dini, asasi za kiraia na wasanii wawili akiwemo mwanamuziki Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz.

Baraza hilo litakaloongozwa na Mwenyekiti wake Leodeger Chilla Tenga, rais wa zamani wa TFF.

Rais pia amemteua Zuwena Mohamed (Shilole) na Faraja Nyarandu wajumbe wa baraza hilo.


Akimwakilisha Rais Samia katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani leo Jumanne, Aprili25, 2023 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema baraza hilo lina jukumu la kukusanya rasilimali fedha kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo kwa lengo la kufikia O Malaria ifikapo 2030.

Akitambulisha wajumbe wengine wa Baraza hilo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemtaja Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigilu Nchemba, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

Naibu Katibu Mkuu Tamisemi anayeshughulikia afya, Dk Wilson Mahera Charles, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk Jimy Yonazi, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Hassan Abbas na Angelina Ngalula na Mwenyekiti Umoja wa mabenki Tanzania, Theobald Sabi.

Amesema pia Rais amemteua Makamu wa Rais wa Anglo Gold Ashanti, Simon Shayo, mfanyabiashara Salim Bakhresa, Askofu Mkuu wa KKKT, Frederick Shoo, Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zuberi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya, Gervas Nyaisonga, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa Foundation BMF, Dk Ellen Senkoro.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments